MAAFA YATOKEA DAR...GOROFA LAPOROMOKA NA KUSABABISHA VIFO







Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam, akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
SOURCE: jestina blog

From Around The Blog

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...